Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:52

Wananchi watoa heshima zao za mwisho kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza

Gari la kubebea maiti lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth II linawasili katika Ikulu ya Holyroodhouse, kabla ya kuelekea kwenye Kanisa Kuu la St Giles, huko Edinburgh, Scotland, Uingereza Septemba 11, 2022. (Reuters).

Wananchi walitoa heshima zao Jumanne kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza katika Kanisa Kuu la St. Giles huko Edinburgh, huku wengi wakisubiri  usiku kucha kupata fursa ya mwisho ya kupita mbele ya jeneza la Malkia kabla ya kusafirishwa kwa ndege hadi London.

Princess Anne anatarajiwa kuandamana na jeneza kwenye ndege ya kurudi London baadaye Jumanne.

Mwili wa malkia kwanza utapelekwa kwenye kasri ya Buckingham, na kisha kuhamishwa kwa maandamano ya umma yatakayoongozwa na Mfalme Charles hadi Ukumbi wa Westminster wa karne ya 11, ambapo utalala kwa siku nne. Ukumbi utakuwa wazi saa 23 kwa siku kwa wageni. Utalindwa na askari wa nyumba ya kifalme.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kusafiri hadi Westminster kutoa heshima zao.

XS
SM
MD
LG