Ajali hiyo ilipelekea gari lake kutoka barabarani huko California, kugonga mti na kushuka kilimani kwa kasi na Woods kujeruhiwa vibaya.
Woods, mwenye umri wa miaka 45, alitolewa katika eneo la ajali na wafanyakazi wa uokoaji na kukimbizwa na gari la wagonjwa kutoka eneo la ajali Jumanne asubuhi nje ya Los Angeles hadi Kituo cha Matibabu cha UCLA.
Kituo hicho cha afya kiko karibu na eneo la alali. Wood alikuwa amepata majeraha mengi ya mguu kwa mujibu wa wakala wake.
Taarifa iliyowekwa kwenye akaunti rasmi ya Twitter ya Woods Jumanne usiku ilisema alikuwa amefanyiwa upasuaji uliochukuia muda mrefu kwenye mguu wake wa kulia na kifundo cha mguu na alikuwa macho wakati wote huo na anaendelea kupata ahueni katika chumba chake cha hospitali.