Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 12:19

Papa Francis awaambia waumini washikamane na Ukraine


Papa Francis katika mkutano wake na hadhara wa kila wiki huko Vatican Picha na Reuters.
Papa Francis katika mkutano wake na hadhara wa kila wiki huko Vatican Picha na Reuters.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis alituma ujumbe wa mshikamano na Ukraine wakati mashambulizi ya Russia katika mji wa Bakhmut na mikoa mingine yakiwa yameongezeka.

Kundi la mamluki la Russia la Wagner lilitangaza mafanikio mapya katika mapambano katika mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine mwishoni wiki. Kinachooneka kama picha za majengo yaliyoharibiwa na timu ya mashambulizi ya mamluki walioko huko, ambapo VOA imeshindwa kupata uthibitisho huru, pia zilitolewa na shirika la habari la Russia la Ria Novosti.

Majeshi ya Ukraine yanahisi shinikizo, mwanajeshi mmoja wa Ukraine aliyejitambulisha kwa jina moja tu Mikhail ameliambia shirika la habari la Associated Press.

“Ni vigumu kuitetea ngome ya Bakhmit kwasababu majeshi mengi ya adui yako hapa. Na pia, hali ya hewa haituruhusu kutumia magari. Matope mengi sana,” amesema Mikhail.

Licha ya changamoto, wanajeshi hawawezi kumudu kupoteza lengo lao, aliongezea kamanda wa kikosi cha 44 ambaye jina limeandikwa ni Gray.

Kamanda “Gray” amesema “Tuna kazi nyingi za kufanya, hakuna kupumzika, wakati wote tuko kazini. Tunafanya kazi hata usiku tukiitwa.”

Mashambulizi ya Russia yamechukua idadi kubwa ya raia, alisema Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, wakati akilihutubia taifa. “Makombora na silaha, drones na mizinga. Taifa adui linatumia silaha tofauti lakini wakiwa na lengo moja tu kichwani. Kuharibu maisha na kutoa chochote kwa binadamu.”

Majeruhi kwa upande wa raia na uharibifu wa nyumba kwa makombora na silaha mbali mbali pia yameripotiwa na polisi wa Ukraine katika mji wa Konstiantynivkwa, magharibi mwa Bakhmut.

Katika mkoa wa kusini la Kherson, watu watatu waliuawa katika mashambulizi. Galyna Kolisnyk alisema shambulizi limetokea wakati alipokuwa dukani. “Milipuko ilianza, gari yetu iliharibiwa, watu walikuwa wameumizwa. Tulikuwa dukani wakati huo.”

Huku ghasia zikiwa zimesambaa, Papa Francis alirejea wito wake wa amani. Wacha tusema tuungane katika Imani na mshikamano na kaka zetu ambao wanataabika kwasababu ya vita. Mbali ya yote hayo, msiwasahamu watu wa Ukraine waliojitoa mhanga.”

Ujumbe wa mshikamano ulisikika kwa maelfu ya watu ambao walikusanyika katika eneo la St. Peter’s Square kushiriki katika sala ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG