Hospitali za muda zimeundwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na janga, lakini wizara ya afya inasema juhudi hizo hazitoshi.
Wafanyakazi wa nchi hiyo wanasemekana wamechoka sana, huku miili ya wagonjwa waliofariki ikiwa imeachwa kwenye vitanda hospitalini kutokana na ukosefu wa wafanyakazi kuiondoa.
Idadi ya wagonjwa katika nchi mablimbali za Afrika inaongezeka huku Shirika la Afya Duniani WHO likionya kwamba hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi.
Kuna upungufu mkubwa wa chanjo kwenye bara hilo, hata hivyo WHO inaeleza matumaini kwamba msaada kutoka Marekani na mataifa mengine kupitia mpango wake wa COVAX utazisaidia nchi hizo katika kampeni zao za kutoa chanjo.