Kupitia mpango wa mfumo huo wa kuchunguza aina mbali mbali ya virusi vipya, Kemri itaweza kutumia vifaa na kemikali za Uingereza ili kuongeza uwezo wa nchi kuchunguza, kupata ushauri wa kifundi na mafunzo.
Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Marriot alisema ushirikiano huo utaimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili.
Waziri wa Afya wa Kenya Muthai Kagwe alifurahia ushirikiano huo ambao alitia saini pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Dominic Raab mwezi Januari.