"Ufaransa ishindwe! Ufaransa, iondoke," waandamanaji hao waliimba, wakirudia kauli mbiu zilizosikika katika mikutano mbalimbali, tangu mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 26 mwezi Julai.
Utawala wa kijeshi wa Niger, Ijumaa uliishutumu Ufaransa, kwa kile ulichokiita"uingiliaji wa wazi" wa masuala ya ndani ya nchi hiyo, kwa kumuunga mkono rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum.
Tangu wakati huo, maelfu ya watu wameshiriki maandamano kwenye mzunguko wa barabara, karibu na kambi ya kijeshi ya Niger, ambapo wanajeshi wa Ufaransa wamekita kambi.
Uhusiano na Ufaransa, mshirika wake katika mapambano dhidi ya ugaidi, ulizorota haraka baada ya Paris kusimama na Rais aliyeondolewa madarakani.
Tarehe 3 mwezi Agosti, serikali ilitangaza sitisho la makubaliano ya kijeshi na Ufaransa, ambayo ina wanajeshi wapatao 1,500 walioko nchini humo.
Forum