Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:11

Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema afariki dunia


Mwenyekiti wa chama cha TLP na mwanasiasa mkongwe  nchini Tanzania  Augustino Lyatonga Mrema wakati wa uhai wake.
Mwenyekiti wa chama cha TLP na mwanasiasa mkongwe  nchini Tanzania  Augustino Lyatonga Mrema wakati wa uhai wake.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha TLP na mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania  Augustino Lyatonga Mrema amefariki dunia  Jumapili, Agost 21, 2022,  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Aminieli Eligaisha amewaambia waandishi wa habari kwamba Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti Jumapili asubuhi.

Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.

Enzi za uhai wake, Mrema aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, akichuana na Hayati Benjamin Mkapa baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Tanzania.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la Mwananchi

XS
SM
MD
LG