Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:00

Mvua kubwa na mafuriko yaua watu 15 magharibi mwa China


Watu wakiendelea kuokolewa katika kitongoji cha Wanzhou, Wilaya ya Chongqing, nchini China, Julai 4, 2023. (China News Service photo via Reuters)
Watu wakiendelea kuokolewa katika kitongoji cha Wanzhou, Wilaya ya Chongqing, nchini China, Julai 4, 2023. (China News Service photo via Reuters)

Shirika la habari la serikali ya China Xinhua linasema watu 15 wamefariki na wengine wanne hawajulikani waliko kutokana na siku kadhaa za mvua kubwa huko  kusini magharibi mwa China.

Vifo hivyo vilitokea katika mji wa Chongqing, ambako mvua zimesababisha mafuriko makubwa yaliyowalazimisha watu wengi kuhama makazi yao yaliyofurika maji na kuzoa magari na kuvunja madaraja.

Shirika la habari la Xinhua linasema mvua na mafuriko yamevuruga maisha ya watu zaidi ya 130,000.

Rais Xi Jinping ameagiza mamlaka husika katika ngazi zote za serikali kulipa suala hili kipaumbele kwa “kuhakikisha usalama watu na mali,” kulingana na Xinhua.

Wizara ya fedha imetenga zaidi ya dola milioni 44 kwa ajili ya mfuko wa msaada wa dharura kwa ajili ya Chongqing na maeneo jirani.

Maeneo mengi nchini China yameathiriwa na mvua kubwa na maporomoko ya matope katika wiki za hivi karibuni, huku viwango vya joto vimepanda zaidi nyuzi 35 Celsius.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya Reuters, AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG