Kadhalika amekiri kuwa yeye (mwenyekiti) hakuingilia kati kuzuia kuenezwa kwa madai hayo, kulingana na maelezo ya ushahidi uliowekwa wazi Jumatatu.
Madai hayo na jinsi kampuni ilivyoshughulikia hayo katikati ya kesi ya kashfa dhidi ya kituo kikubwa cha habari iliyowasilishwa na Dominion Voting Systems.
Nyaraka zilizofunguliwa hivi karibuni ikiwemo maelezo kutoka katika ushahidi ambao Murdoch alihojiwa juu yake iwapo alikuwa anafahamu kuwa baadhi ya watangazaji wa mtandao huo – Lou Dobbs, Maria Bartiromo, Jeanine Pirro na Sean Hannity – katika baadhi ya nyakati walithibitisha madai ya uongo ya uchaguzi. Murdoch alijibu, “Ndiyo. Walithibitisha hivyo.”
Ushahidi wa Murdoch ni wa hivi karibuni kuwasilishwa katika kesi ya kashfa ikionyesha wasiwasi katika mtandao uliokuwa na hadhi ya juu namna ulivyoshughulikia madai ya Trump wakati viwango vyake vikiporomoka baada ya kituo hicho kutangaza Joe Biden ameshinda Arizona, ikimkasirisha Trump na wafuasi wake.