Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:13

China huenda ikaishambulia Taiwan kuanzia 2027 - CIA


Mkuu wa idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA), William Burns.
Mkuu wa idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA), William Burns.

Mkuu wa idara ya Ujasusi ya Marekani, CIA, William Burns, amesema Jumapili kwamba ripoti za kijasusi zinaonyesha kuwa rais wa China Xi Jinping ameamuru jeshi lake liwe tayari kushambulia Taiwan kufikia mwaka wa 2027.

Burns hata hata hivyo, amesema huenda Xi ans wasiwasi kuhusu hatua kama hiyo, kutokana na hali iliyokumba Russia baada ya kushambulia Ukraine.

Burns wakati akiwa kwenye mahojiano ya televisheni Jumapili amesema kwamba Marekani lazima ichukulie azma ya la Xi ya kuchukua udhibiti kamili wa Taiwan kwa uzito, hata kama itamaanisha nguvu za kijeshi kutumika.

Kwenye mahojiano hayo ya kwenye kipindi cha “Face The Nation” cha kituo cha televisheni cha CBS, Burns amesema kwamba wanafahamu kuwa taarifa imetolewa kwa umma kuhusu agizo la rais Xi kwa jeshi la China kwamba liwe tayari kushambulia Taiwan kufikia mwaka wa 2027, lakini haina maana kwamba ameamua kufanya hivyo.

Taiwan na China zilitengana mwaka wa 1994 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, chama cha Kikomunisti kikiachiwa utawala wa China bara. Hata ingawa kisiwa cha Taiwan kinajitawala, bado hakijatambuliwa kama taifa na Umoja wa Mataifa au taifa lingine kubwa.

Mwaka 1979, rais wa Marekani Jimmy Carter alitambua rasmi serikali ya Beijing wakati akitamatisha uhusiano wa kitaifa na Taiwan. Kwa kujibu, bunge la Marekani lilipitisha sheria ya uhusiano na Taiwan ya kuendeleza ushirikiano na kisiwa hicho.

Rais wa Marekani Joe Biden ameweka bayana kwamba Marekani ipo tayari kulinda Taiwan iwapo China itaishambulia. Ukulu ya Marekani imesema kwamba sera ya Marekani haijabadilika, na kwamba Washington ingetaka kuona suala la Taiwan likisuluhishwa kwa njia ya amani.

Hata hivyo, haijasema lolote kuhusu iwapo Marekani iko tayari kutuma vikosi vyake iwapo Taiwan itashambuliwa

XS
SM
MD
LG