Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:12
VOA Direct Packages

Taiwan kuimarisha zaidi uhusiano wa kijeshi na Marekani


Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen akiwa na ujumbe wa Marekani mjini Taipei.
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen akiwa na ujumbe wa Marekani mjini Taipei.

Rais wa Taiwan Tsai Ing –wen amesema kwamba kisiwa hicho kinachojitawala kiatendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na Marekani.

Kiongozi huyo ameyasema hayo mapema Jumanne wakati akifanya kikao na wabunge wa Marekani walioko ziarani kwenye mji mkuu wa Taipei. Amesema kwamba Taiwan itaongeza ushirikiano na Marekani pamoja na mataifa mengi ya kidemokrasia ili kukabiliana na chamgamoto kama vile mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na mataifa yenye ushawishi wa kipebari.

Mwaka 1979 Marekani ilibadili utambuzi wa kidiplomasia wa China kutoka Taiwan hadi Beijing ingawa inaendelea kuipatia Taiwan vifaa vya kijeshi kwa ajili ya kujilinda, kwa mujibu wa makubaliano ya mahusiano na kisiwa hicho.

Beijing huiona Taiwan kama sehemu yake ingawa imekuwa ikijitawala tangu mwisho mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China vilivyomalizika 1949, pale vikosi vya Chiang Kai-shek vilipoondolewa China bara na wakomunisti wa Mao Zedong.

China imeapa kurejesha udhibiti wa kisiwa hicho kwa namna yoyote ile ikiwemo kupitia njia ya kijeshi. Mwakilishi wa Marekani Ro Khanna ambaye ni mmoja wa wajumbe huru kwenye kamati maalum ya Marekani inayotathmini ushindani kati ya China na Marekani, na anayeongoza ujumbe wa Marekani wa Taiwan, ameambia Tsai wamekuja kudhibitisha uhusiano uliopo kati ya Marekani na Taiwan.

XS
SM
MD
LG