Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni zaidi kidogo ya wiki moja baada ya China kuahidi kujibu mapigo kwa Marekani, baada ya kutungua puto ambalo linaaminika kufanya upelelezi ambalo liliruka katika sehemu kubwa ya Marekani.
Katika taarifa, wizara ya biashara ya China, imesema kampuni za Lockheed Martin Corp, na Raytheon Technologies Corp, na kitengo chake cha makombora na ulinzi kwa pamoja vimepigwa marufuku kujihusisha na uingizaji ama usafirishaji unaohusiana na China ama kufanya uwekezaji wowote mpya nchini humo.
Kampuni zote hizo zinakatazwa na sheria za Marekani kuuza silaha zinazohusiana na teknolojia za China.