Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:19

Blinken azungumza na waziri ajaye wa mambo ya nje wa China


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, alizungumza na waziri wa mambo ya nje wa China ajaye, Qin Gang, kwa njia ya simu Jumapili.

Blinken alichukua hatua hiyo baada ya China wiki iliyopita kumteua balozi wake wa Marekani kuwa waziri mpya wa mambo ya nje.

Waziri Blinken amesema alijadiliana naye kuhusu uhusiano wa Marekani na China na kudumisha mawasiliano.

China siku ya Ijumaa ilimteua Qin, balozi wake nchini Marekani na msaidizi wa kutumainiwa wa Rais Xi Jinping, kuwa waziri wake mpya wa mambo ya nje, huku Beijing na Washington zikijaribu kuleta utulivu wa mahusiano.

Qin, 56, anachukua nafasi ya Wang Yi, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa muongo mmoja uliopita.

Wang, mwenye umri wa miaka 69, alipandishwa cheo katika chama cha kikomunisti cha China mwezi Oktoba na anatarajiwa kuchukua nafasi kubwa zaidi katika sera ya mambo ya nje ya China.

XS
SM
MD
LG