Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:40

Maelfu waandamana Mexico kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi


Waandamanaji washiriki maandamano ya kupinga mpango wa Rais Manuel Lopez Obrador wa kurekebisha mamlaka ya uchaguzi, mjini Mexico, Februari 26, 2023
Waandamanaji washiriki maandamano ya kupinga mpango wa Rais Manuel Lopez Obrador wa kurekebisha mamlaka ya uchaguzi, mjini Mexico, Februari 26, 2023

Maelfu ya waandamanaji walifurika eneo la biashara maarufu kama Plaza la Mexico City Jumapili kupinga mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yanayopendekezwa na Rais Andres Manuel Lopez Obrador ambayo wanasema yanatishia demokrasia na yanaweza kuashiria kurudi kwenye hali mbaya ya miaka ya nyuma.

Eneo la Plaza kawaida linaaminika kupokea karibu watu 100,000, lakini waandamanaji wengi ambao hawakuweza kuingia katika eneo hilo walikusanyika kwenye mitaa ya karibu na eneo hilo.

Waandamanaji wengi walikuwa wamevalia mavazi ya rangi ya taasisi ya kitaifa ya uchaguzi, wakipaza sauti na kusema “ Usibadili kura yangu”.

Madabiliko ya sheria ya uchaguzi yamepelekea Marekani kueleza msimamo wake.

Brian A. Nichols, waziri mdogo wa Marekani anayehusika na masuala ya kanda ya magharibi, ameandika kwenye Twitter “Leo huko Mexico, tunashuhudia mjadala mkubwa kuhusu mageuzi ya uchaguzi ambayo ni mtihani kwa uhuru wa taasisi za uchaguzi na mahakama.”

“Marekani inaunga mkono taasisi huru za uchaguzi zenye uwezo wa kutosha ambazo zinaimarisha michakato ya kidemokrasia na utawala wa sheria,” Nichols aliandika.

Mapendekezo ya Rais Obrador yalipitishwa wiki iliyopita. Ikiwa yataanza kutekelezwa, yatapunguza mishahara, fedha za ofisi za uchaguzi wa mitaa na mafunzo kwa waninchi wanaofuatilia na kusimamia uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura. Yatapunguza pia adhabu kwa wagombea wanaoshindwa kuripoti matumizi ya kampeni zao za uchaguzi.

XS
SM
MD
LG