Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:10

Marekani yasema haitambui unyakuzi wa Russia wa Peninsula ya Crimea


Basi likivuka juu ya daraja linalounganisha Russia na Crimea Februari 14, 2023.REUTERS.
Basi likivuka juu ya daraja linalounganisha Russia na Crimea Februari 14, 2023.REUTERS.

Marekani ilitangaza Jumapili kwamba Peninsula ya Crimea inasalia kuwa sehemu ya Ukraine lakini ikasema wasiwasi wa haraka zaidi ni kwa vikosi vya Kyiv kuchukua  tena ardhi ambazo Moscow imeziteka katika vita vyake vya mwaka mzima.

Marekani haitambui na kamwe haitatambua unyakuzi wa Russia wa peninsula hiyo. Crimea ni Ukraine, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa yake.

Wakati huo huo, Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Rais Joe Biden, alikambia kipindi cha Meet the Press cha kituo cha televisheni cha NBC kwamba ni juu ya Ukraine kuamua nini kinajumuisha ushindi au matokeo yanayokubalika ya kidiplomasia, ingawa hakuna mazungumzo ya amani yanayofanyika.

Hiyo ni juu ya Ukraine kufafanua, Sullivan alisema. Imekuwa muhimu kwetu kwamba hakuna chochote kuhusu Ukraine bila Ukraine. Na hivyo, si juu ya Marekani kueleza maana ya ushindi kwa Ukraine. Ni juu ya Marekani kuiunga mkono Ukraine kwenye uwanja wa vita, ili waweze kupata ushindi waliouainisha aliongeza.

XS
SM
MD
LG