Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:36

Mkuu wa viwanda vya kuoka mikate Tunisia awekwa mbaroni


Wateja wakinunua mikate katika duka la kuoka mikate huko Ariana, Tunisia Mei 22, 2023. Picha na REUTERS/Jihed Abidellaoui
Wateja wakinunua mikate katika duka la kuoka mikate huko Ariana, Tunisia Mei 22, 2023. Picha na REUTERS/Jihed Abidellaoui

Mamlaka nchini Tunisia imemkamata mkuu wa chama cha kitaifa cha wamiliki wa viwanda vya kuoka mikate, kwa tuhuma za "ukiritimba" wakati nchi hiyo inakabiliwa na uhaba ruzuku ya mkate kwa muda wa wiki moja, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Alhamisi.

Mwezi Agosti, Serikali ilipiga marufuku baadhi ya viwanda vya watu binafsi 1,500 vya kuoka mikate ambavyo vinazalisha mikate na maandazi katika mtindo wa nchi za Ulaya wakinunua unga wa ruzuku, hivyo kukomesha tabia iliyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja.

Ruzuku inabakia kutumika kwa viwanda vya uokaji 3,737 na mtandao mwingine unaouza mkate kwa bei iliyoidhinishwa na serikali, ambayo haijabadilika tangu mwaka 1984.

Mkuu wa chama cha waoka mikate Mohamed Bouanane alikamatwa Jumatano "kwa tuhuma za ukiritimba na uvumi wa vyakula vya ruzuku" na utakatishaji pesa, vyombo vya habari vya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini vimeripoti.

Kampuni binafsi za kuoka mikate ziliingia katika mgomo Agosti 7, zikidai makubaliano kutoka wizara ya biashara, zikihoji kuondolewa kwa ruzuku kungelazimisha baadhi ya viwanda kufungwa.

Ghasia za mkate za mwaka 1983 hadi 1984 nchini Tunisia zilisababisha vifo vya watu zaidi ya 150.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG