Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:24

Miili mitano ya wahamiaji yapatikana katika eneo lisilo na watu karibu na mpaka kati ya Libya na Tunisia


Vijana wa Tunisia wafunga barabara ya wahamiaji kwa kuchoma moto matairi huko Sfax, Julai 4, 2023. Picha na shirika la habari la AFP.
Vijana wa Tunisia wafunga barabara ya wahamiaji kwa kuchoma moto matairi huko Sfax, Julai 4, 2023. Picha na shirika la habari la AFP.

Miili mitano ya wahamiaji walioko kusini mwa jangwa la Sahara imepatikana katika eneo lisilo na watu karibu na mpaka kati ya Libya na Tunisia, wizara ya mambo ya ndani ya Libya ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatatu.

Wizara hiyo ilisema kuwa miili hiyo ilipatikana wakati wakifanya doria karibu na maeneo ya mpaka na Tunisia kati ya Dahra na Tawilat Al-Rutba.

Darzeni ya Waafrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara wamekwama karibu na mpaka wa Libya na wanasema kuwa maafisa wa Tunisia waliwaondoa na kuwaleta katika eneo hili la mpaka kutoka mji wa Sfax mapema mwezi huu.

Baadaye serikali ya Tunisia iliwahamishia kwenye makazi ya muda katika miji miwili lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu yalisema kwamba darzeni ya watu bado wamekwama huko katika hali ngumu sana wameachwa na kiu na njaa katika wimbi la joto ambalo halijawahi kutokea.

Forum

XS
SM
MD
LG