Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:33

Wahamiaji wanne wafariki dunia na wengine  51 hawajulikani walipo


Wahamiaji kutoka Ivory Coast, kundi la Waafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaonekana wamekwama kwenye ufuo unaodaiwa kuwa kwenye mpaka wa Tunisia na Libya Alhamisi Julai 6, 2023.
Wahamiaji kutoka Ivory Coast, kundi la Waafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaonekana wamekwama kwenye ufuo unaodaiwa kuwa kwenye mpaka wa Tunisia na Libya Alhamisi Julai 6, 2023.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inakabiliwa na wimbi kubwa la uhamiaji mwaka huu

Takriban wahamiaji wanne walifariki dunia na wengine 51 hawajulikani walipo baada ya meli yao kuzama kwenye kisiwa cha Kerkennah nchini Tunisia afisa wa mahakama aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumapili akiongeza kuwa wahamiaji wote waliokuwa ndani ya meli hiyo wanatoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Walinzi wa pwani ya Tunisia walipata miili 901 ya wahamiaji waliokufa maji katika pwani yake kuanzia Januari mosi hadi Julai 20 mwaka huu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo alisema mwezi Julai na kuashiria idadi kubwa ya waathirika katika pwani ya nchi hiyo.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inakabiliwa na wimbi kubwa la uhamiaji mwaka huu na maafa ya mara kwa mara ya boti za wahamiaji kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaoelekea katika pwani ya Italia kuzama.

Tunisia imechukua nafasi ya Libya kama kitovu kikuu cha kanda hiyo kwa watu wanaokimbia umaskini na migogoro barani Afrika na Mashariki ya Kati kwa matumaini ya maisha bora barani Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG