Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:26

Tunisia na Libya zawachukua wahamiaji 276 waliokwama katika eneo la jangwa


Wahamiaji kutoka Afrika wameketi chini huku wakiwa wamekwama kwenye jangwa kati ya mpaka wa Libya na Tunisia, karibu na Al-Assah. REUTERS
Wahamiaji kutoka Afrika wameketi chini huku wakiwa wamekwama kwenye jangwa kati ya mpaka wa Libya na Tunisia, karibu na Al-Assah. REUTERS

Pwani ya Tunisia haswa mji wa bandari wa mashariki wa Sfax  hivi karibuni umechukua nafasi ya Libya kama sehemu kuu ya wahamiaji wa Kiafrika

Tunisia na Libya ziliwachukua wahamiaji 276 waliokwama katika eneo la jangwa kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili na kuwalepeleka kwenye makazi siku ya Alhamisi.

Tunisia imelaumiwa kwa kuwatupa wahamiaji hao kwenye joto kali katika ardhi isiyo na mtu karibu na kituo cha mpaka cha Ras Jedir. Libya ilisema Jumatano kwamba wahamiaji 27 kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara walikutwa wamekufa na maafisa wa Libya katika jangwa la magharibi karibu na mpaka wa Tunisia.

Pwani ya Tunisia haswa mji wa bandari wa mashariki wa Sfax hivi karibuni umechukua nafasi ya Libya kama sehemu kuu ya wahamiaji wa Kiafrika wanaosafiri kwa boti chakavu kuelekea Ulaya kuvuka Bahari ya Mediteranian.

Tulichukua jukumu la kundi lililokuwa limehifadhiwa na Hilali Nyekundu ya Tunisia na upande wa Libya ulifanya vivyo hivyo ili wahamiaji hao waondolewe katika eneo hilo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia Faker Bouzghaya aliiambia Associated Press.

Forum

XS
SM
MD
LG