Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:32

Tunisia na Libya zatangaza kukubaliana kutoa hifadhi kwa wahamiaji waliokwama mpakani


Wahamiaji wenye asili ya Kiafrika wakiwa wamejazana katika boti dogo huku walinzi wa pwani ya Tunisia wakijitayarisha kuwahamisha katika chombo kingine salama, katika eneo la bahari kati ya Tunisia na Italia Aug. 10, 2023.
Wahamiaji wenye asili ya Kiafrika wakiwa wamejazana katika boti dogo huku walinzi wa pwani ya Tunisia wakijitayarisha kuwahamisha katika chombo kingine salama, katika eneo la bahari kati ya Tunisia na Italia Aug. 10, 2023.

Tunisia na Libya wametangaza hivi leo kuwa wamekubaliana kushirikiana na wajibu wa kutoa hifadhi kwa mamia ya wahamiaji ambao wamekwama mpakani, wengi wao kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Wahamiaji, kimsingi kutoka nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, wamesukumwa kwenda kwenye eneo la jangwani la Ras Jedir na maafisa wa Tunisia na kuwaacha huko wakijikimu wenyewe, kwa mujibu wa walioshudhuia, makundi ya kutetea haki na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Khadija Riyami anaisoma ripoti kamili.

Mashirika ya misaada yamesema makundi matatu ya takriban wahamiaji 300 kutoka nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara kwa ujumla walikwama huko na kuishi katika hali ya kutishia maisha yao.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia, Faker Bouzghaya, alisema wakati wa kikao cha pamoja na maafisa wa Libya mjini Tunis kwamba “tumekubaliana kushirikiana makundi haya ya wahamiaji ambao wako mpakani. “

“Tunisia itachukua jukumu la kundi la wanaume 76, wanawake 42 na watoto wanane,” Bouzghaya aliliambia shirika la habari la AFP.

Alisema makundi yalihamishwa siku ya Jumatano na kupelekwa kwenye vituo katika miji ya Tatouine na Medenine na kupatiwa huduma za afya na kisaikolojia, kwa msaada wa shirika la Mwezi Mwekundu la Tunisia.

Kwa mujibu wa makubaliano, Libya itachukua kundi lililobaki la wahamiaji kati ya 150 na 200, vyanzo vya mashirika ya kibinadamu vilisema.

Wizara ya mambo ya ndani ya Libya mapema Alhamisi ilitangaza kufikiwa kwa mkataba wa pande mbili wa “kumaliza mzozo wa wahamiaji wasio wa kawaida waliokwama kwenye eneo la mpakani.”

Katika taarifa yake baadaye, ilisema kulikuwa hakuna wahamiaji zaidi waliokwama kwenye mpaka kufuatia makubaliano hayo, ikiongezea kwamba doria za pamoja zimeandaliwa ili “kulilinda eneo la mpakani.”

Mivutano ya rangi imeongezeka nchini Tunisia katika mji wa Sfax baada ya mauaji ya Julai 3 ya mwanamme mmoja raia wa Runisia kufuatia ugomvi na wahamiaji.

Mpaka waafrika weusi 1,200 walifukuzwa, au kuondolewa kwa nguvu na majeshi ya usalama ya Tunisia, na kupelekea kwenye mikoa ya jangwani kwenye mpaka na Libya na Algeria, Human Rights imesema.

Shirika la Mwezi Mwekundu tunia Julai 12 liliwapatia makazi kiasi cha wahamiaji 630 waliogundulika huko Ras Jedir, pamoja na wengine 200 ambao walisukumwa kuelekea Algeria, makundi yasiyo ya kiserikalli yalisema.

Lakini waandishi wa habari wa AFP na vyombo vingine vya habari waliripoti kwamba kiasi cha wahamiaji 350 bado wamekwama huko Ras Jedir katika wiki zilizofuata.

Kasi cha kilometa 40 kusini mwa Al Assah, mamia ya wahamiaji wengine walionekana kumiminika kuingia nchini Libya, huku wakiwa hawana fursa ya chakula, maji na wala mahitaji muhimu mpaka walipookolewa na walinzi wa mpakani wa Libya mapema mwezi Agosti, kwa mujibu wa timu ya AFP iliyokuwa huko.

Tangu kuanza kwa mwezi Julai, “kiasi cha wahamiaji 27” waligundulika wamefariki baada ya kuachwa katika eneo la mpakani kati ya Tunisia na Libya na wengine 73 hawajulikani walipo, chanzo cha kibinadamu kimeiambia AFP leo Alhamisi.

Mpaka siku ya Jumatano wahamiaji waliendelea kuwasili nchini Libya huko Al Assah kwa kiwango cha kiasi watu 50 kwa siku kabla ya kuokolewa na walinzi wa Libya, chanzo hicho kimesema.

Nchi mbili za Afrika Kaskazini ni njia kuu kwa wahamiaji na waomba hifadhi wanaojaribu kufanya safari hatari kwa kutumia boti chakavu kwa matumaini ya kutafuta maisha bora huko Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG