Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:18

Italia yazialika nchi za Mediterania kwa ajili ya mkutano unaolenga kuongeza  mkataba wa kuzuia wahamiaji


Ajali mbaya ya meli iliyobeba wahamiaji katika ufukwe wa Crotone mashariki Februari 26,2023.(REUTERS)
Ajali mbaya ya meli iliyobeba wahamiaji katika ufukwe wa Crotone mashariki Februari 26,2023.(REUTERS)

Italia ilizialika nchi za Mediterania mjini Roma jana Jumapili kwa ajili ya mkutano wa kimataifa unaolenga kuongeza  mkataba unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya na Tunisia ili kuzuia kuingia  kwa wahamiaji kwenye fukwe za Ulaya.

Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni anatarajia viongozi kutoka kwenyhe eneo hilo la Umoja wa Ulaya na taasisi za kimataifa za fedha zitakutana katika mji mkuu kwa mujibu wa taarifa ya serikali kwenye vyombo vya habari.

Orodha kamili ya washiriki haijajulikana lakini Meloni amethibitisha kuwepo kwa Rais wa Tunisia Kais Saied huku mawaziri wakuu wa Misri na Malta Mostafa Madbouli na Robert Abela wote kwa pamoja wamesema watahudhuria.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022 uliomuingiza madarakani Meloni aliapa kusimamisha uingiaji wa wahamiaji nchini Italia ambao serikali ilitaja kuwa karibu watu 80,000 waliofika pwani tangu Januari ikilinganishwa na 33,000 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita

Forum

XS
SM
MD
LG