Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:27

Mke wa Kizza Besigye asema hatarajii mahakama ya kijeshi kumtendea haki mumewe


Winnie Byanyima, mke wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye. Picha na Reuters
Winnie Byanyima, mke wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye. Picha na Reuters

Mke wa mwanasiasa maarufu nchini Uganda Winnie Byanyima, ambaye mumewake alikamatwa katika nchi jirani ya Kenya amesema mwishoni mwa wiki kwamba hatarajii kuwa mume wake atapata haki katika mahakama ya kijeshi ambako ameshitakiwa.

Kizza Besigye alikamatwa Novemba 16 na watu wasiojulikana kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi ambako alikwenda kuhudhuria uzinduzi wa kitabu na kulazimishwa kurejea Kampala.

Baadae alishtakiwa katika mahakama ya kijeshi kwa makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria.

Besigye alikuwa mmoja wa washirika wa karibu na daktari wa rais Yoweri Museveni wakati kiongozi huyo mwenye umri mkubwa alipokuwa msituni akipambana na serikali wakati huo. Washirika hao wawili baadae walitofautiana kabla Besigye kustaafu jeshini na kushindana na Museveni mara nne katika nafasi ya urais . alipoteza ushindi mara zote lakini alidai matokeo yameibwa.

Upinzani nchini Uganda na makundi ya kutetea haki mara nyingi yameshutumu serikali ya Museveni kwa kutumia Mahakama ya jeshi kuadhibu wapinzani wa upinzani wa rais. Winnie Byanyima amesema mashitaka hayo yana ushawishi wa kisiasa.

“Nitazungumza na kila mtu. Ndiyo, nina hamu ya kuzungumza na rais, kuzungumza na viongozi kama wanataka, viongozi wengine, iwe ndani ya bunge au popote kuhusu jinsi ya kusonga mbele, kwa sababu hii siyo tu kwa ajili ya Besigye,” amesema Byanyima

“Hii ni kuhusu jinzi upinzani unavyoweza kuwa na nafasi yake, nafasi nzuri ya kutekelez ajukumu lake katika demnokrasia ya kikataiba,” ameongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG