Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:29

Kenya ilihusika pakubwa kukamatwa kwa Besigye; anasema Wakili Erias Lukwago


Kizza Besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda.
Kizza Besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda.

Kenya ilisisitiza haihusiani na kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani na mkosoaji wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Wakili wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda alisema Jumamosi kwamba inaonekana mamlaka za Kenya ilihusika pakubwa katika kukamatwa kwa Kizza Besigye na kumuondoa nchini kinyume cha sheria jijini Nairobi.

Uganda inakabiliwa na ukosoaji wa kimataifa kufuatia kutekwa kutoka mji mkuu wa Kenya kwa kiongozi mkongwe wa upinzani Besigye, ambaye alifikishwa katika mahakama ya Kampala siku ya Jumatano.

Kenya ilisisitiza kuwa haihusiani na kukamatwa kwa kiongozi huyo mwenye miaka 68, ambaye ana taaluma ya daktari wa binadamu na mkosoaji wa muda mrefu wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Inaonekana kuna amri kutoka serikali ya Kenya katika utekaji nyara wa Besigye hadi kupelekwa kwake kinyume cha sheria nchini Uganda, Wakili Erias Lukwago aliliambia shirika la habari la AFP.

Alisema alipata nyaraka za Besigye kutoka Nairobi licha ya idara ya ujasusi ya Kenya kumkatalia kufika katika chumba cha hoteli ambako Besigye alikaa kabla ya tukio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG