Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 07:04

Kiongozi wa upinzani Uganda Besigye akamatwa Kenya


Uganda Opposition Leader
Uganda Opposition Leader

Mwanasiasa maarufu wa upinzani wa Uganda alikamatwa wakati wa uzinduzi wa kitabu nchini Kenya mwishoni mwa wiki  na kusafirishwa hadi Uganda, anashikiliwa katika jela ya  kijeshi mjini Kampala, mke wake amesema leo katika mtandao wa kijamii wa X.

Kizza Besigye amekuwa mpinzani wa rais Yoweri Museveni kwa muda mrefu katika chaguzi nne na kushindwa mara zote, ingawa alipinga matokeo akishutumu kulikuwa na wizi wa kura na vitisho kwa wapiga kura. Amekamatwa mara nyingi kabla ya sasa.

Msemaji wa jeshi la Uganda hakupatikana mara moja kutoa maoni yake, wakati msemaji wa jeshi la polisi la Kenya pia naye hakujibu haraka alipotafutwa kutoka maoni yake, shirika la habari la ROITA limesema.

Mwezi Julai maafisa wa usalama wa Kenya waliwakamata wanachama 36 wa chama cha siasa cha Besigye -FDC ambacho ni kikubwa nchini Uganda miongoni mwa makundi ya upinzani ambako walishitakiwa kwa ugaidi.

Besigye ambaye alikuwa daktari wa Museveni wakati wa vita vya msituni na baadae alikuwa mkosoaji mkubwa wa kiongozi huyo , alitekwa Jumamosi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha mwanasiasa wa upinzani Martha Karua , mke wake Winnie Byanyima ameandika katika mtandao wa X.

Hata hivyo serikali ya Museveni imeshutumiwa mara kadhaa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya viongozi wa upinzani na wafuasi wao , ikiwemo kuwafunga kinyume cha sheria , mateso na mauaji holela. Maafisa wamekanusha shutuma hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG