Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:28

Vifo vimefikia 24 kutokana na mlipuko wa lori la mafuta nchini Uganda


Mfano wa lori la mafuta lililopata ajali huku watu wakipita pembeni bila kuhofia usalama wao. Nigeria. Oct. 16, 2024.
Mfano wa lori la mafuta lililopata ajali huku watu wakipita pembeni bila kuhofia usalama wao. Nigeria. Oct. 16, 2024.

Uganda imeshuhudia visa hivyo huku watu wakikimbilia kuiba mafuta kutoka kwenye malori yaliyopata ajali barabarani.

Idadi ya vifo kufuatia mlipuko wa lori la mafuta karibu na mji mkuu wa Uganda Kampala wiki iliyopita imeongezeka na kufikia 24, serikali imesema leo Jumapili.

Nchi hiyo maskini ya Afrika Mashariki imeshuhudia majanga kadhaa kama hayo katika miaka ya hivi karibuni, huku watu wakikimbilia kuiba mafuta kutoka kwenye malori ya mafuta yaliyopata ajali barabarani.

“Ajali mbaya iliyotokea Jumanne katika mji wa Kigogwa, takriban kilomita 25 kaskazini mwa Kampala, iliripotiwa kuwa watu 11 walifariki katika eneo la tukio”, alisema Waziri wa Mawasiliano Godfrey Kabbyanga katika taarifa yake.

Aliongeza kuwa watu wengine 13 wamefariki dunia katika hospitali ya Kiruddu na hospitali ya jeshi ya Bombo na kufikisha idadi ya vifo 24”. Kwa kuwa baadhi ya waliofariki waliungua sana na moto na kushindwa kutambuliwa, polisi wamekuwa jitihada kubwa kumtambua kila marehemu kupitia uchunguzi wa DNA, alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG