Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:41

Misri, Marekani na washirika wengine wapanga jinsi ya kufikisha misaada Gaza


Moshi ukifuka baada ya shambulio la roketi kutoka Gaza katika mji ulioko Kusini mwa Israel wa Ashkelon, Oktoba 11, 2023. Picha na Picha na RONALDO SCHEMIDT / AFP.
Moshi ukifuka baada ya shambulio la roketi kutoka Gaza katika mji ulioko Kusini mwa Israel wa Ashkelon, Oktoba 11, 2023. Picha na Picha na RONALDO SCHEMIDT / AFP.

Misri imejadili mipango na Marekani na nchi nyingine kupitisha misaada ya kibinadamu kupitia mpaka wake na Ukanda wa Gaza, chini sitisho la muda mfupi la mapigano, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vilisema siku ya Jumatano.

Misaada huenda ikapitia katika kivuko mpakani cha Rafah kati ya Gaza na Peninsula ya Sinai ya Misri, vyanzo vilisema, vilipokuwa vikizungumza kwa misingi ya kutotajwa.

Wakati huo huo shirika la habari la AFP limeripoti mwanadiplomasia wa juu wa Misri Sameh Shoukry alikuwa mwenyeji wa mazungumzo na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) Philippe Lazzarini siku ya Jumatano wakati ghasia zikisambaa katika ujirani wa Gaza ambao zimewakosesha makazi zaidi ya watu 263,000.

Mazungumzo ya Shoukry na mkuu wa UNRWA yalilenga "jinsi ya kutoa ulinzi kwa raia na kuhakikisha upatikanaji wa mara kwa mara wa huduma na misaada kwa Gaza," wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa yake.

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa utaratibu wa amani wa Mashariki ya Kati, Tor Wennesland, pia alihudhuria mkutano huo.

Shoukry alionya kuhusu "hali ya hatari ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza" na kusema Misri "inaunga mkono kikamilifu mashirika ya Umoja wa Mataifa" katika kuhakikisha upelekaji wa misaada ya kibinadamu.

Njia pekee ya kuingia Gaza isiyodhibitiwa na Israel ni kivuko cha Rafah kutoka Misri, ambacho ndege za Israel zilipiga mabomu mara tatu kati ya Jumatatu na Jumanne.

Tangu wanamgambo wa Hamas waanzishe mashambulizi ya kikatili ya kuvuka mpaka kutoka Gaza siku ya Jumamosi, Israel imekuwa ikilishambulia eneo hilo kwa mashambulizi ya anga.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG