Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:51

Israel yafanya mashambulizi Gaza huku idadi ya vifo kwa pande zote ikiongezeka


Uharibifu wa mashambulizi ya anga ya Israel katika Jiji la Gaza, Jumatano, Oktoba 11, 2023. (Picha ya AP/Adel Hana).
Uharibifu wa mashambulizi ya anga ya Israel katika Jiji la Gaza, Jumatano, Oktoba 11, 2023. (Picha ya AP/Adel Hana).

Maafisa wa afya wa Palestina walisema Jumatano idadi ya waliofariki Gaza iliongezeka hadi watu 1,055, huku wengine zaidi ya 5,000 wakijeruhiwa.

Israel ilishambulia barabara na majengo katika Ukanda wa Gaza kwa mashambulizi ya anga Jumatano wakati ikiongoza kampeni ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio la wanamgambo wa Hamas ambalo limesababisha vifo vya takriban watu 1,200 nchini Israel.

Maafisa wa afya wa Palestina walisema Jumatano idadi ya waliofariki Gaza iliongezeka hadi watu 1,055, huku wengine zaidi ya 5,000 wakijeruhiwa tangu Israel ifanye mashambulizi yake ya kwanza saa chache baada ya mashambulizi ya Hamas kuanza Jumamosi.

Makundi ya misaada ya kibinadamu yameelezea hofu kuhusu hali ya raia huko Gaza huku kukiwa na ahadi ya Israel ya kuwazuia watu milioni 2.3 kuweza kupata maji, chakula na umeme.

Mamlaka ya nishati ya Gaza ilieleza Jumatano inatazamia kukosa mafuta kwa ajili ya mtambo wake pekee wa kuzalisha umeme baadaye jumatano. Madaktari Wasio na Mipaka walisema mafuta na vifaa vya matibabu vinaendelea kupungua.

Katika ujumbe wa video mapema Jumatano, msemaji wa jeshi la Israel Luteni Kanali Jonathan Conricus alitetea mashambulizi ya anga ya Israel ambayo yameharibu majengo ya makazi ya watu akisema maeneo hayo ni malengo halali ya kijeshi kwa sababu Hamas inaweka makusudi operesheni zake katika majengo ya kiraia.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 263,000 wamekimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza tangu mapigano yaanze, na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

Forum

XS
SM
MD
LG