Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:50

Milipuko katika miji miwili ya Somalia yaua watano


Ramani ya Somalia
Ramani ya Somalia

Kundi la al-Shabaab linalojihusisha na kundi la kigaidi la Al- Qaida limesema limetekeleza mashambulizi hayo mawili.

Katika tukio la kwanza, mabomu mawili yalitegwa katika soko la mifugo kwenye mji wa Afgoye katika jimbo la Lower Shabelle yameuwa angalau watu wanne polisi na wakaazi wamesema.

Bomu moja lililipuka lakini halikusababisha vifo, baadae bomu la pili lililipuka na kuuwa raia wanne, kapteni wa polisi Nur Farah ameliambia shirika la habari la ROITA kutoka Afgoye.

Mlipuko wa pili katika mji wa bandari wa Marka ulimuuwa kamishna wa wilaya, radio ya serikali imesema.

Katika mtandao wa twitter radio hiyo imeaandika kuwa “ kamishna wa wilaya ya Marka , mji mkuu wa jimbo la Lower shabelle , Abdullahi Ali Wafow ameuwawa katika shambulizi la kigaidi kwenye mji.”

XS
SM
MD
LG