Waziri wa habari Saleban Yusuf aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu wa jimbo hilo la kaskazini magharibi, Hargeisa kwamba” BBC ilishindwa kuitambua Somaliland kama nchi ya kidemokrasia iliyosimama imara kwa miaka 30.
“Kuanzia leo, nimeamuru shughuli zote zinazohusiana na BBC nchini Somaliland zisitishwe,” amesema.
“Masikio ya wanainchi wa Somaliland hayastahili taarifa ambazo BBC inatumia kuielezea Somaliland,” ameongeza.
Somaliland ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka wa 1991 na imestawi kama mwanga unaolinganishwa wa uthabiti, lakini haitambuliwi kidiplomasia na taifa lingine lolote.
BBC inatangaza taarifa za habari katika lugha ya Kisomali na ina mtandao wa waandishi wa habari wanaofanya kazi nchini kote Somalia, ikiwemo mjini Hargeisa.