Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:58

Rais mpya wa Somalia aapishwa, viongozi wa Afrika wahudhuria


Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud

Viongozi kutoka Djibouti, Ethiopia, Kenya na Misri wamehudhuria sherehe za  kuapishwa rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud zilizofanyika mjini Mogadishu.

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Djibouti ulioongozwa na rais Ismail Guelleh, televisheni ya taifa ya SNTV imesema katika mtandao wake wa twitter na kutoa picha za Bwana Guelleh na ujumbe wake.

Televisheni ya taifa pia imebandika picha katika twitter ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwasili Mogadishu kwa ajili ya sherehe hizo.

Rais wa kenya uhuru Kenyatta pia alipokelewa katika uwanja wa ndege wa Mogadishu na waziri mkuu wa somalia Mohamed Hussein Roble.

Hali ya usalama iliongezwa katika mji mkuu na mji huo ambao awali uliweka amri ya kutotoka nje kabla ya mkutano huo.

Rais wa somalia aliapishwa May 15 haraka baada ya kuchaguliwa na bunge. Mrithi wake alikabidhi madaraka May 23.

XS
SM
MD
LG