Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:46

Takriban nusu ya wakazi wa Somalia kwenye hatari ya njaa


Mnyama aliyekufa kutokana na ukame,Somalia.
Mnyama aliyekufa kutokana na ukame,Somalia.

Mjumbe wa masuala ya huduma za dharura wa Somalia amesema takriban nusu ya raia wa Somalia wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na ukame, huku baadhi ya maeneo ya nchi yakikabiliwa na hatari ya njaa.

Akizungumza kwenye mkutano mjini Mogadishu , Abdurahman Abdishakur Warsame, alisema kuwa Zaidi wa wasomali millioni sita wanakabiliwa na ukame, na kwamba idadi ya watu wanaotaabika inaendelea kuongezeka na kufikia takriban nusu ya raia wa taifa hilo.

Warsame alisema kuwa ukame umeathiri takriban wilaya 72 kati ya wilaya 84 za Somalia, na kwamba sita kati ya hizo tayari zinakabiliwa na njaa na hali ngumu za ukosefu wa usalama wa chakula.

Hali inayoshuhudiwa inasemekana kuwa mbaya zaidi kutokea kwenye taifa hilo katika kipindi cha miaka 40, na tayari imepelekea wasomalia takriban laki saba kukimbia maeneo ya mashambani na kuelekea kwenye miji ya karibu.
Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yameonya Jumanne kwamba tishio la njaa linaongezeka huko Somalia na katika nchi jirani za Ethiopia na Kenya.

XS
SM
MD
LG