Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:40

Milionea wa DRC awasilisha ombi lake la kugombea urais


Mgombea Urais wa chama cha upinzani cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi (katikati) akiwapungia mkono wafuasi wake huko Lubumbashi Mei 11, 2016. Picha na REUTERS/Kenny Katombe
Mgombea Urais wa chama cha upinzani cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi (katikati) akiwapungia mkono wafuasi wake huko Lubumbashi Mei 11, 2016. Picha na REUTERS/Kenny Katombe

Kiongozi wa upinzani wa Congo Moise Katumbi amewasilisha ombi lake la kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Desemba ambapo Rais Felix Tshisekedi anawania tena nafasi hiyo kwa muhula wa pili, chama chake kilisema siku ya Jumatano.

Katumbi, mfanyabiashara tajiri mkubwa na gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga wenye utajiri wa shaba, pia atashindana dhidi ya Martin Fayulu - ambaye aliibuka mshindi wa pili katika uchaguzi uliopita - na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya magonjwa ya wanawake Denis Mukwege na wengineo.

Tshisekedi, ni mtoto wa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Congo Etienne Tshisekedi, muhula wa kwanza wa utawala wake umekumbwa na msukosuko ymatatizo ya kiuchumi, milipuko ya magonjwa na kuongezeka kwa mashambulizi ya wanamgambo katika eneo la Mashariki.

"Nchi yetu haijahukumiwa kwa vita, wala ukosefu wa usalama, wala kwa utawala mbaya, au kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria na uhuru," Katumbi alisema katika taarifa hiyo.

Chama chake cha Ensemble pour la Republique katika wiki zijazo kitatangaza mpango wake ambao utalenga kurejesha usalama, kutengeneza ajira na kuboresha huduma za kijamii.

Wakati Tshisekedi alipoingia madarakani akiahidi kumaliza miongo kadhaa ya ukandamizaji wa kisiasa na rushwa, makundi ya haki, washirika wa kimataifa na wapinzani wanamshutumu kwa kuwa mgandamizaji sawa na wale waliomtangulia.

Forum

XS
SM
MD
LG