Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 04:15

Waliouawa katika msako mkali kuwahi kufanyika Mashariki mwa DRC wazikwa


Wafanyakazi wa makaburi yaliyoko nje ya mji wa Goma, huko DRC wakijianda kwa mazishi Septemba 18, 2023. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP.
Wafanyakazi wa makaburi yaliyoko nje ya mji wa Goma, huko DRC wakijianda kwa mazishi Septemba 18, 2023. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP.

Harufu ya miili iliyooza ilisambaa hewani wakati wafanyakazi wa makaburini huko mashariki mwa Congo waliposhusha darzeni ya majeneza kuwazika waathirika wa moja ya maandamano mabaya zaidi katika kumbukumbu za eneo hilo za hivi karibuni.

Watu wasiopungua 56 waliuawa tarehe 30 mwezi Agosti, kulingana na mwendesha mashtaka wa jeshi, baada ya wanajeshi wa Congo mjini Goma kuwafyatulia risasi waandamanaji kabla ya maandamano kuanza ya kupinga uwepo wa walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa.

Mahakama ya kijeshi siku ya Jumatatu iliwahukumu baadhi ya washtakiwa hao kwa kupanga umwagaji damu, na serikali ililipia mazishi na kuwalipa fidia waombolezaji na familia zilizokuwa na hasira.

Wengi wanahangaika kukubaliana na hali ya kuwapoteza wapendwa wao . "Ni uhalifu, kwakile walichokifanya," alisema mjane mwenye umri wa miaka 26 Tumaini Barumana Biluge, waliliamikia wiki mbili ambapo yeye na waombolezaji wengine walilazimika kusubiri ili kutambua maiti ya waathirika.

"Hatukuweza tena kutambua sura za watu, jamaa waliwatambua ndugu zao tu kwa nguo walizokuwa wamevaa," alisema akiwa katika nyumba yake ya kawaida katika kitongoji cha Goma, siku moja baada ya mazishi ya Septemba 18.

Kaka wa mume wake pia aliuawa tarehe 30 Agosti. Yeye na wifi yake, Zawadi Balthazar mwenye umri wa miaka 22, sasa lazima awalee watoto sita bila ya baba zao. Wote walilia waliporudi kuzuru makaburi tarehe 19 mwezi Septemba.

Jumatatu, wanajeshi watatu kati ya sita walioshtakiwa kwa jukumu lao katika mauaji hayo walihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, huku mkuu wa kitengo cha Walinzi wa Jamhuri mjini Goma alihukumiwa adhabu ya kifo, ambayo inatarajiwa kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha.

Watuhumiwa wengine wawili waliachiliwa huru.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG