Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:56

Miili minane yatambuliwa katika ajali ya jengo la ghorofa Florida


Mume na mke wakionyesha majonzi yao katika eneo ambalo jumba liliporomoka wakati waokoaji wakiendelea na zoezi la kutafuta miili, karibu na pwani ya Florida, Marekani, Juni 26, 2021. REUTERS/Marco Bello
Mume na mke wakionyesha majonzi yao katika eneo ambalo jumba liliporomoka wakati waokoaji wakiendelea na zoezi la kutafuta miili, karibu na pwani ya Florida, Marekani, Juni 26, 2021. REUTERS/Marco Bello

Maafisa wa afya wamewatambua watu wanane kati ya tisa waliothibitishwa wamefariki kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa 12 la ufukweni huko Florida.

Zaidi ya watu wengine 150 bado hawajulikani walipo wakati waokoaji wakiendelea na zoezi la kuwatafuta kwenye vifusi vya jengo la Champlain Towers.

Shirika la Habari la Associated Press limekuwa likiripoti maelezo mafupi ya waathiriwa.

Waliopotea ni pamoja na wanafamilia watatu wa familia ya Wamarekani wenye asili ya Cuba ya Mora wa Cuba na wakili Linda March, ambaye nyumba yake ya juu kabisa iliathirika wakati jengo hilo lilipoanguka.

Polisi walisema waliofariki pia ni pamoja na Stacie Dawn Fang, ambaye mtoto wake wa kiume mchanga alinusurika; Manuel LaFont, mhandisi ambaye alifanya kazi kufanya barabara kuu kuwa salama; na Antonio na Gladys Lozano, ambao hivi karibuni walifikia miaka 59 ya ndoa yao.

XS
SM
MD
LG