Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:55

Jengo lililoanguka Florida lilianza kutitia tangu 1990; vyanzo vya habari vinaripoti


Sehemu ya jengo lililoanguka Florida nchini Marekani
Sehemu ya jengo lililoanguka Florida nchini Marekani

Mhandisi wa majengo aliona hitilafu ya nyufa na sehemu za kuta zinabomoka, nguzo sio imara katika sehemu za kuegeshea magari zilizopo chini ya jengo hilo. Ripoti pia ilisema uharibifu kwa sehemu kubwa kwenye maeneo muhimu unahitajika kutengenezwa kwa wakati

Gazeti la New York Times la Marekani linaripoti Jumamosi kwamba ripoti ya mhandisi wa majengo iliyotoka miaka mitatu iliyopita juu ya jengo lenye ghorofa 13 lenye makaazi ya kuishi katika jimbo la Florida huko kusini mwa Marekani ambalo lilianguka Alhamis ilieleza kwamba misingi ya jengo hilo ilikua na kasoro na uharibifu mkubwa.

Mhandisi huyo aliona hitilafu ya nyufa na sehemu za kuta zinabomoka, nguzo sio imara katika sehemu za kuegeshea magari zilizopo chini ya jengo hilo, kulingana na gazeti hilo. The Times ilisema kwamba ripoti hiyo ndio ilikua sababu ya kutayarisha ukarabati wa mamilioni ya dola ambao ulipangwa kuanza hivi karibuni.

Gazeti hilo lilisema maafisa wa manispaa walitoa ripoti ya mhandisi mwishoni mwa Ijumaa. Ripoti ya mwaka 2018 haikutoa ushahidi wowote kwamba jengo hilo lilikuwa karibu kuanguka lakini ilisema uharibifu kwa sehemu kubwa kwenye maeneo muhimu unahitajika kutengenezwa kwa wakati.

Muonekano wa jengo lililoanguka Florida, Marekani
Muonekano wa jengo lililoanguka Florida, Marekani

Wakati huo huo gazeti la Washington Post la nchini Marekani ilitoa mfano wa utafiti uliofanywa mwaka 2020 na iliripoti kuwa jengo hilo lilijengwa kwenye ardhi yenye unyevunyevu au maji kwenye ukingo wa kisiwa ambacho kinaunda eneo la Miami Beach. Taarifa iliendelea pia jengo hilo limekuwa likititia tangu miaka ya 1990. Haijulikani bado ikiwa sababu hizo zilichangia tukio hilo kutokea.

XS
SM
MD
LG