Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:40

Mazishi ya mkuu wa Wagner yafanyika kwa faragha


Picha ya mkuu wa mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin kwenye kumbukumbu ya muda iliyoko Moscow, Agosti 24, 2023. Picha na REUTERS/Stringer.
Picha ya mkuu wa mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin kwenye kumbukumbu ya muda iliyoko Moscow, Agosti 24, 2023. Picha na REUTERS/Stringer.

Mazishi ya mkuu wa mamluki wa Russia Yevgeny Prigozhin, ambaye aliuawa katika ajali ya ndege wiki iliyopita, yamefanyika kwa faragha kwenye makaburi yaliyoko nje kidogo ya mji aliotoka wa St Petersburg, chombo chake cha habari kimesema Jumanne.

"Kuagwa kwa Yevgeny Prigozhin kulifanyika kwa faragha. Wale wanaotaka kumuaga wanaweza kutembelea makaburi ya Porokhovskoye," chombo hicho cha habari kimesema katika chapisho fupi kwenye Telegram, ikiambatana na picha ya Prigozhin.

Usiri ulikuwa umezingira mipango ya mazishi ya Prigozhin, ambaye aliuawa katika ajali ya ndege Agosti 23, miezi miwili kuanzia siku alipoanzisha uasi uliosababisha changamoto kubwa sana tangu utawala wa rais Vladimir Putin uingie madarakani mwaka 1999.

Awali Ikulu ya Kremlin ilikuwa imesema kuwa Putin hatahudhuria mazishi hayo.

"Uwepo wa rais haukutarajiwa," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari.

Watu wengine wawili wakuu wa kundi hilo la Wagner, walinzi wanne wa Prigozhin na wafanyakazi watatu pia waliuawa wakati ndege binafsi ya kiongozi huyo wa Wagner aina ya Embraer Legacy 600 ilipoanguka kaskazini mwa Moscow.

Putin wiki iliyopita alielezea Prigozhin kama mtu aliyefanya alifanya "makosa makubwa maishani mwake, lakini amepata matokeo sahihi."

Ikulu ya Kremlin imekanusha uvumi kwamba Putin ilipanga ajali hiyo kama kulipiza kisasi kwa maandamano ya Wagner yaliyofanyika Juni mjini Moscow.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG