Putin alisaini amri hiyo inayoleta mabadiliko na ilianza kutekelezwa siku ya Ijumaa, baada ya Kremlin kusema kwamba madai ya nchi za Magharibi kuwa Prigozhin aliuawa kwa amri yake ni “uongo mtupu”.
Mamlaka ya usafiri wa ndege ya Russia ilisema kwamba Prigozhin alikuwa ndani ya ndege binafsi iliyoanguka Jumatano jioni kaskazini magharibi mwa Moscow na hakuna abiria aliyenusurika katika ajali hiyo, ambayo ilitokea miezi miwili baada ya Prigozhin kuongoza uasi uliofeli dhidi ya wakuu wa jeshi.
Rais Putin alituma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki katika ajali hiyo siku ya Alhamisi na kumzungumzia Prigozhin katika zama zilizopita.
Putin kuweka kiapo cha lazima kwa wafanyakazi wa kundi la Wagner na wakandarasi wengine wa jeshi binafsi ilikuwa hatua ya wazi ya kuweka makundi kama hayo chini ya udhibiti mkali wa serikali.
Forum