Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:53

Rais Erdogan kuzuru Russia kujadili kuvunjika kwa makubaliano ya nafaka


Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan ataitembelea Russia hivi karibuni kujadili kuvunjika  kwa makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa yaliyoruhusu usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia bahari ya Black Sea, msemaji wa Chama tawala cha Uturuki cha  AK alisema Jumatatu.

Makublaiano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturukiy yalidumu kwa mwaka mmoja lakini yalimalizika mwezi uliopita baada ya Moscow kujitoa. Ankara inatafuta njia ya kuishawishi Russia kurejea katika mkataba huo, ambapo bandari kadhaa katika mji wa Odesa zilikuwa zikisafirisha mamilioni ya tani za nafaka.

Tangu makubaliano ya usafirishaji wa nafaka kuvunjika, majeshi ya Russia yamekuwa yakilenga bandari za Ukraine kwa kuzishambulia vikali na makombora na droni za kamikaze.

Omer Celik, msemaji wa Chama cha AK, alisema Erdogan atafanya ziara katika eneo la mapumziko la Sochi kwenye bahari ya Black Sea “karibuni” lakini hakueleza iwapo atakutana na Rais wa Russia Vladimir Putin.

“Baada ya ziara hii huenda yakawepo maendeleo na hatua mpya kufikiwa kuhusiana na suala hili” makubaliano ya usafirishaji nafaka, aliwaambia waandishi.

Kremlin ilisema Ijumaa kuna maelewano kuwa viongozi hao wawili watakutana ana kwa ana hivi karibuni.

Kampuni ya habari ya Bloomberg ilieleza vyanzo viwili ambavyo havijatajwa majina katika ripoti yao kuwa Erdogan anatarajiwa kukutana na Putin nchini Russia wiki ijayo, pengine Septemba 8, kabla hajasafiri kuelekea katika mkutano wa viongozi wa G20 nchini India.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG