Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:13

Romania kuongeza maradufu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine


Meli za mizigo zikiwa kwenye bandari ya Romania ya Constanta
Meli za mizigo zikiwa kwenye bandari ya Romania ya Constanta

Romania imepanga kuongeza maradufu usafirishaji wa nafaka za Ukraine hadi kwenye bandari yake ya Constanta iliyoko kwenye bahari ya Black Sea.

Taifa hilo limepanga kufikia tani milioni 4 katika miezi ijayo, na hasa kwa kutumia njia ya mto Danube, amesema waziri wa Uchukuzi Sorin Grindeanu.

Ukraine ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza ulimwenguni katika upelekaji wa nafaka, lakini Russia imekuwa ikiharibu ghala zake pamoja na miundombinu ya bandari baada ya kukataa kuongeza muda wa mkataba ulioiruhusu Ukraine kupeleka nafaka kwenye mataifa ya nje kupitia Black Sea.

Mkataba huo ulikuwa umefadhiliwa na UN na Uturuki. Baadhi ya bandari za Ukraine zilizoshambuliwa katika siku za karibuni ni pamoja na zile za eneo la Danube za Reni na Izmail.

Forum

XS
SM
MD
LG