Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:43

Canada yasema kwamba uhalifu wa kimitandao unahujumu usalama wa taifa pamoja na uchumi


Mtaalam wa masuala ya kupambana na udukuzi Stuart Davis akiwa mbele ya ramani ya Iran akieleza wanahabari kuhusu uhalifu wa kimitandao
Mtaalam wa masuala ya kupambana na udukuzi Stuart Davis akiwa mbele ya ramani ya Iran akieleza wanahabari kuhusu uhalifu wa kimitandao

Idara ya kitaifa ya ujasusi ya Canada imesema Jumatatu kwamba uhalifu wa kimitandao unatishia usalama wa kitaifa na ustawi wa kiuchumi kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Kupitia ripoti yake, idara ya Communications Security Establishment CSE imetaja Russia na Iran kama mataifa yanayotoa mazingira salama kwa wahalifu wa kimitandao kushambulia mataifa ya magharibi. Mashambulizi ya kimitandao kwenye miundombinu muhimu kama vile hospitali na mabomba ya mafuta yanaweza kusababisha hasara kubwa kulingana na ripoti hiyo.

Imeongeza kusema kwamba wahalifu wa kimitandao wameendelea kuonyesha ustahimilifu pamoja na uwezo wa kuwa wabunifu kwenye shughuli zao. Udukuzi wa aina ya Ransomware umetajwa kuwa tishio kubwa zaidi kwa Canada kutokana na kuenea kwake, na huenda ukaathiri uwezo wa mashirika makubwa kutekeleza majukumu yao.

Takwimu rasmi zinaonyesha kwamba 2022 kulikuwa na mashambulizi 70,878 nchini Canada wakati zaidi ya dola milioni 390 zikiibiwa. Mratibu mkuu wa idara ya kitaifa ya kupambana na udukuzi ya Canada Chris Lynam amesema kwamba ni visa vichache sana vilivyoripotiwa mwaka jana, na kwa hivyo huenda mabilioni ya dola yalipotea.

Forum

XS
SM
MD
LG