Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 04:51

Mashtaka dhidi ya Trump yatasomwa rasmi mbele ya Baraza la Seneti


Spika wa Baraza la Wawakilishi akisaini azimio la kufikisha mashtaka mawili dhidi ya Rais Donald Trump
katika Baraza la Seneti, Jumatano, Januari 15, 2020.
Spika wa Baraza la Wawakilishi akisaini azimio la kufikisha mashtaka mawili dhidi ya Rais Donald Trump katika Baraza la Seneti, Jumatano, Januari 15, 2020.

Baraza la Seneti la Bunge la Marekani kwa mara ya tatu katika historia ya nchi hii litasikiliza kesi dhidi ya rais, baada ya kupokea rasmi Jumatano mashtaka mawili kutoka Baraza la Wawakilishi dhidi ya Rais Donald Trump.

Mashataka hayo yatasomwa Alhamisi mbele ya baraza la maseneta 100, ambao baada ya kuapishwa Alhamisi, wanageuka kuwa wajumbe wa baraza la kutoa maamuzi kwenye shauri hilo, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Marekani John Roberts.

Mashtaka hayo yaliidhinishwa na kutiwa saini na Spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi Jumatano kabla ya kupelekwa mbele ya baraza la Seneti.

Nancy Pelosi amesema "leo tumeweka historia wakati waendesha mashtaka watapeleka katika hatua ya kihistoria mashtaka dhidi ya rais wa Marekani kwa kutumia vibaya madaraka yake na kuzuia bunge kufanya kazi yake.

Pelosi amewateua wajumbe saba wa baraza lake ili kuwa waendesha mashtaka wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya upelelezi Adam Shiff.

Wademokrats watajaribu kudhihirisha kwamba Rais Trump alitumia vibaya madaraka yake kwa kuhimiza uingiliaji kati wa kigeni katika uchaguzi wa 2020, pale alipokuwa ana zungumza kwa simu Julai 25 na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelinskiy.

Wakati huo alimtaka kiongozi huyo kumfanyia uchunguzi mpinzani wake mkuu makamu rais wa zamani Joe Biden.

Changamoto kubwa hivi sasa ni ikiwa kiongozi wa waliowengi katika baraza la seneti Mitch McConnell na Warepublikan watakubali madai ya wademoktrats kusikiliza mashahidi muhimu na ushahidi mpya ulojitokeza hivi sasa.

XS
SM
MD
LG