Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:41

Marekani : Watano wapoteza maisha – Gari lavamia na kugonga gwaride la Krismas


Polisi wafunga mtaa huko mji wa Waukesha, Wisconsin, baada ya gari kuvamia na kuwagonga watu waliokuwa katika gwaride la Krismas, Jumapili, Nov. 21, 2021. (AP Photo/Jeffrey Phelps)
Polisi wafunga mtaa huko mji wa Waukesha, Wisconsin, baada ya gari kuvamia na kuwagonga watu waliokuwa katika gwaride la Krismas, Jumapili, Nov. 21, 2021. (AP Photo/Jeffrey Phelps)

Gari aina ya SUV lilivamia gwaride la krismasi, huko Waukesha, katikla jimbo la Wisconsin hapa Marekani Jumapili na kuua watu watano na kujeruhi wengine zaidi ya 40, ikiwemo kundi la wacheza dansi waliokuwa wakipeperusha maua.

Mkuu wa Polisi wa Waukesha, Dan Thompson alisema mtu mmoja amekamatwa na yuko chini ya ulinzi na gari pia limepatikana baada ya tukio mjini humo, kiasi cha kilometa 32 magharibi mwa Milwaukee.

Dan Thompson, Mkuu wa Polisi wa Waukesha anasema : “ Gari liliwagonga zaidi ya watu 20. Baadhi ya watu hao walikuwa watoto na kuna wengine wamejeruhiwa vibaya zikiwa ni matokeo ya tukio hilo. Hatutatoa habari zaidi kuhusu majeruhi kwa wakati huu wakati tunafanya jitihada za kuwajulisha wana familia wa wale waliofariki.”

Maafisa huko Waukesha wameonya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka na majeruhi wanaweza kubadilika wakati habari za ziada zikiendelea kukusanywa.

Wamesema baadhi ya watu walijipeleka wenyewe katika hospitali za eneo.

Gwaride la Waukesha, kwenye jamii ya takriban watu 72,000, linafanyika kila mwaka Jumapili kabla ya sikukuu ya Thanksgiving na linajumuisha kuvaa mavazi maalum, wacheza dansi, na bendi kushiriki katika gwaride. Kauli mbiu yam waka huu ili ni “faraja na furaha.”

XS
SM
MD
LG