Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:35

Makubaliano yamefikiwa kati ya jeshi na viongozi wa kiraia nchini Sudan


Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (L) and Waziri Mkuu Abdalla Hamdok
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan (L) and Waziri Mkuu Abdalla Hamdok

Abdalla Hamdok ataongoza baraza la mawaziri huru la kiufundi, maafisa walisema. Walisema UN, Marekani na wengine walishiriki katika majukumu muhimu ya kuunda makubaliano

Makubaliano yamefikiwa kati ya wanajeshi na viongozi wa kiraia wa Sudan kumrejesha kwenye uongozi Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok ambaye aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya mwezi uliopita maafisa wa jeshi na serikali walisema Jumapili.

Pia walisema kwamba maafisa wa serikali na wanasiasa waliokamatwa tangu mapinduzi ya Oktoba 25 wataachiliwa huru kama sehemu ya makubaliano kati ya jeshi na vyama vya siasa kikiwemo chama kikubwa cha Umma Party.

Hamdok ataongoza baraza la mawaziri huru la kiufundi, maafisa walisema. Walisema UN, Marekani na wengine walishiriki katika majukumu muhimu ya kuunda makubaliano. Walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kujadili makubaliano hayo kabla ya kutangazwa rasmi.

Mapinduzi hayo zaidi ya miaka miwili baada ya vuguvugu la wananchi kumuondoa kwa nguvu madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir na serikali yake ya ki-Islam kumesababisha ukosoaji wa kimataifa. Marekani, washirika wake na Umoja wa Mataifa wanalaani matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi.

XS
SM
MD
LG