Pia wamesema maafisa wa serikali na wanasiasa waliokamatwa tangu mapinduzi ya Oktoba 25 wataachiliwa ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya jeshi na vyama vya siasa, kikiwemo chama kikubwa cha Umma Party.
Hamdok ataongoza Baraza la Mawaziri la kiufundi lililohuru, maafisa wamesema. Wamesema UN, Marekani na wengine walikuwa na “majukumu muhimu” katika kuandaa makubaliano hayo. Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kujadili makubaliano hayo kabla ya tangazo rasmi.
Mapinduzi hayo, baada ya zaidi ya miaka miwili kufuatia vuguvugu maarufu la kisiasa lililomuondoa madarakani mtawala wa muda mrefu Omar al-Bashir na serikali yake ya Kiislam, lilikosolewa kimataifa. Marekani, washirika wake na Umoja wa Mataifa walillaani matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi.
Wasudani wamekuwa wakijitokeza mitaani kwa wingi tangu jeshi lilipochukuwa madaraka, yaliyomaliza hatua tete ya mpito kuelekea demokrasia ya nchi hiyo. Makubaliano hayo yamekuja siku kadhaa baada ya madaktari kusema watu wasiopungua 15 waliuawa kutokana na ufyatuaji wa risasi za moto wakati wa maandamano dhidi ya mapinduzi.
Jeshi limenang’ania madaraka, kwa kuteua, baraza jipya la la kijeshi. Mwenyekiti wa Baraza hilo ni kiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdel-Fattah Burhan.
Baraza hilo litakutana baadae Jumapili kabla ya kutangaza makubaliano, maafisa wamesema.
Hatua ya kitaifa iliyoanzishwa baada ya mapinduzi ikihusisha vyama vya siasa na viongozi wa umma wamesema katika taarifa kuwa Hamdok atarejeshwa katika nafasi yake na kuunda Baraza la Mawaziri la kiufundi. Taarifa imesema makubaliano yatasainiwa baadae Jumapili pamoja na azimio la kisiasa. Haikueleza zaidi.
Nguvu ya Azimio la Uhuru na Mabadiliko, kikundi kilichoanzisha vuguvugu la kisiasa lililofikia kuondolewa madarakani kwa Bashir, limepinga makubaliano yoyote na jeshi.
Katika taarifa yao ya Jumamosi, kikundi hicho kilirejea upinzani wake kwa ushirikiano wowote mpya wa kisiasa na jeshi, wakisisitiza wahusika wa mapinduzi hayo lazima wafikishwe mbele ya sheria.
“Hatuhusiki na makubaliano yoyote yaliyofikiwa na utawala wa katili na tunaendelea kutumia njia zote za amani na ubunifu kuwaondoa madarakani,” tamko hilo limesema.
Kikundi hicho kimerejea tena wito wake kuitisha maandamano ya nchi nzima kupinga utawala wa kijeshi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP