Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:35

Viongozi wa kijeshi Sudan watakiwa kurejesha utawala wa kiraia


Wafuasi wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Sudan cha Umma , wakiandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi Oct. 29, 2021, mjini Omdurman, Sudan.
Wafuasi wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Sudan cha Umma , wakiandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi Oct. 29, 2021, mjini Omdurman, Sudan.

Saudi Arabia na umoja wa falme za kiarabu zimetoa wito wa kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Sudan.

Hii ni hatua ya hivi punde ya kuiongezea Sudan shinikizo la kimataifa kubadilisha mapinduzi ya kijeshi.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Saudi Arabia, Marekani, Uingereza na umoja wa falme za kiarabu, zimetaka Sudan kuwaachilia huru wafungwa wote wanaozuliwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni, pamoja na kuondolewa kwa hali ya dharura nchini humo.

Juhudi kadhaa za mazungumzo ya kimataifa na ndani ya nchi kurejesha hali ya utulivu Sudan, zimekuwa zikifanyika kwa siku kadhaa sasa.

Chanzo cha habari kilicho karibu na Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, kimeambia shirika la habari la Reuters kwamba mazungumzo yanaendelea lakini hakuna makubaliano yamefikiwa hadi sasa.

Ofisi ya Hamdok imesema kwamba Waziri huyo mkuu anataka wafungwa kuachiliwa huru na taasisi za serikali kurejeshewa mamlaka kabla ya mazungumzo muhimu kufanyika na jeshi.

Ofisi yake vile vile imekanusha ripoti kwamba amekubali kuongoza serikali mpya.

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Abdel Fattah al- Burhan, ambaye amesema anataka kurejeshwa na kuundwa kwa serikali ya kiraia alisema jumatano kwamba alikuwa katika mchakato wa kuteua Waziri mkuu.

Amesema kwamba huenda Hamdok akarejea ofisini kuongoza baraza la mawaziri.

XS
SM
MD
LG