Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:13

Huduma za intarnet zaendelea kukosekana Sudan


FILE - Waandamanaji wakiimba na kupinga hatua ya hivi karibuni ya jeshi kurejesha utawala wa kijeshi na kuondoa utawala wa kiraia mjini Khartoum, Sudan, Oct. 30, 2021. REUTERS/Mohamed Nureldin
FILE - Waandamanaji wakiimba na kupinga hatua ya hivi karibuni ya jeshi kurejesha utawala wa kijeshi na kuondoa utawala wa kiraia mjini Khartoum, Sudan, Oct. 30, 2021. REUTERS/Mohamed Nureldin

Huduma ya internet haijarejea nchini Sudan licha ya mahakama kuziamuru kampuni tatu kubwa za mawasiliano kurejesha huduma hiyo.

Sudan ilifunga huduma ya internet Oktoba 25 kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Pia iliuondoa madarakani utawala wa kiraia uliyokuwa unaongoza taifa hilo katika kipindi cha mpito tangu kupinduliwa kwa Omar al-Bashir.

Mahakama moja Jumanne iliamuru kampuni za Zain, MTN na Sudani, kurudisha huduma za internet lakini shirika linalofuatilia uhuru wa matumizi ya internet la Netblocks, limesema kwamba bado hakuna huduma ya internet nchini humo.

Wanaharakati wa kudai mabadiliko, waliofanikiwa kuandaa maandamano ya awali, wamefanikiwa kuandaa maandamano ya kutaka kurejeshwa utawala wa kiraia bila ya kuwepo huduma ya internet. Wameitisha maandamano mengine Jumamosi, Novemba 13.

XS
SM
MD
LG