Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 18:13

Maelfu waandamana katika miji mbalimbali ya Sudan


Maandamano mjini Khartoum.
Maandamano mjini Khartoum.

Darzeni za maelfu ya raia wa Sudan, Jumamosi walifanya  maandamano mjini Khartoum, na miji mingine nchini humo, kudai kurejeshwa kwa serikali inayoongozwa na raia, ili kuirejesha nchi hiyo kwenye njia ya demokrasia, baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Watu walibeba bendera za Sudan na kuimba "Utawala wa kijeshi hauwezi kusifiwa" na "Nchi hii ni yetu, na serikali yetu ni ya kiraia" walipokuwa wakiandamana katika vitongoji mbalimbali vya mji mkuu, Khartoum.

Waandamanaji pia waliingia mitaani katika miji ya kati, mashariki na kaskazini mwa Sudan.

Maelfu ya Wasudan wamekuwa wakiandamana wiki yote, kupinga kuondolewa madarakani kwa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, siku ya Jumatatu na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, katika mapinduzi yaliyopelekea mataifa ya Magharibi kuzuia utoaji wa mamia ya mamilioni ya dola za misaada.

Jumamosi kulishuhudiwa uwepo mkubwa wa wanajeshi wenye silaha, pamoja na maafisa wengine katikati mwa mjia wa Khartoum.

Vikosi vya usalama vilikuwa vimefunga barabara zinazoelekea katika jengo la wizara ya ulinzi na uwanja wa ndege, pamoja na madaraja mengi, yanayounganisha Khartoum na miji yake pacha ya Omdurman na Khartoum Kaskazini.

Takriban waandamanaji 11 wameuawa katika makabiliano na vikosi vya usalama wiki hii, na wapinzani wanahofia ukandamizaji zaidi.

Katika vitongoji mbalimbali, vikundi vya waandamanaji vilifunga barabara usiku kucha kwa mawe, matofali, matawi ya miti na mabomba ya plastiki, ili kujaribu kuzuia vikosi vya usalama kuwafikia.

Mzee wa miaka 75 ambaye alijitaja kama Moatez na ambaye alikuwa akitembea mitaani kutafuta mkate alisema maisha ya kawaida yamesitishwa kabisa huko Khartoum.

"Kwa nini Burhan na jeshi waliiweka nchi katika mgogoro huu? Wangeweza kutatua tatizo bila vurugu,” alisema.

XS
SM
MD
LG