Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:27

Austin : Marekani ina nia ya dhati na uhakika kwa usalama wa Mashariki ya Kati


Waziri wa Ulinzi wa Bahrain Abdulla bin Hasan Al-Nuaimi akimpokea Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, Manama, Nov. 19, 2021(Photo by BNA (Bahrain News Agency) / AFP)
Waziri wa Ulinzi wa Bahrain Abdulla bin Hasan Al-Nuaimi akimpokea Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, Manama, Nov. 19, 2021(Photo by BNA (Bahrain News Agency) / AFP)

“Tunataka iwe wazi : Nia ya dhati ya Marekani kwa usalama huko Mashariki ya Kati ni imara na ya uhakika,” Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema Jumamosi katika Mdahalo wa Manama huko Bahrain.

Maafisa katika eneo hilo wana wasiwasi juu ya ahadi ya Marekani kwa eneo hilo, hususan tangu ilipoanza kutafuta kufikia makubaliano ya nyuklia na Iran na baada ya hatua ya Marekani kuondoka Afghanistan.

“Lakini hatua ya Iran katika miezi ya karibuni siyo yenye kutia moyo – hususan kwa sababu ya kuendelea kwao kupanua programu yao ya nyuklia,” Austin ameongeza.

Hata hivyo, waziri wa ulinzi pia amesema kuwa “marafiki na maadui wote wanajua” uwezo ambao Marekani inaweza kuutumia.

Austin pia ameweka wazi Jumamosi kuwa Marekani inawezekana katafuta suluhu ya kidiplomasia kwa sababu katika uongozi wa Biden, diplomasia “ndio nyenzo ya kwanza kutumika.”

Akimnukuu Rais wa zamani wa Marekani Dwigth Eisenhower, Austin amesema, “silaha peke yake haiwezi kuipa dunia amani ya kudumu.”

XS
SM
MD
LG