Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:23

Marekani na Tanzania kuimarisha uhusiano wao


Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris (Kulia) akiwa na mume wake Douglas Emhoff (kushoto) wakipunga mikono wakati wakipanda ndege kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Lusaka, Zambia. Picha na ERICKY BONIPHACE / POOL / AFP.
Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris (Kulia) akiwa na mume wake Douglas Emhoff (kushoto) wakipunga mikono wakati wakipanda ndege kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Lusaka, Zambia. Picha na ERICKY BONIPHACE / POOL / AFP.

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris anatarajia kumaliza ziara yake katika bara la Afrika siku ya Jumapili akiwa nchini Zambia, ziara ambayo ni sehemu ya msukumo wa kidiplomasia wa Washington wa kuimarisha uhusiano na bara la Afrika ambako ushawishi wa China na Russia unazidi kuongezeka.

Akiwa nchini Tanzania, Kamala Harris alifanya mazungumzo na Tanzania na rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja mbali mbali ikiwemo biashara, mawsiliano na kuipa Tanzania msaada wa takriban dola milioni 560 kwa mwaka ujao wa fedha.

Siku ya Alhamis makamu huyo wa rais wa Marekani alisema taifa hilo litaongeza ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya kiuchumi katika usambazaji wa kiwango cha betri za nikeli kutoka Tanzania kwenda Marekani na katika masoko ya kimataifa, usambazaji huo unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2026.

Aidha Marekani itasaidia katika kutanua na upatikanaji wa mtandao wa intaneti wa bei nafuu, na kuongeza ushirikiano katika maendeleo ya kisiasa, miradi ya afya, uwezeshaji wa wanawake na viumbe hai mbalimbali.

“Asante kwa maendeleo uliyoyafanya katika kipindi cha utawala wako, wewe ni bingwa, umekuwa bingwa katika masuala ya mabadiliko ya kisiasa katika nchi hii, kwa njia hiyo umepanua mahusiano yetu na hivyo leo basi ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi zetu mbili. Na chini ya uongozi wako nina imani kabisa tutaweza kufanya hivyo” alisema Kamala Harris.

Naye rais Samia Suluhu alisema “leo tumepiga hatua nyingine muhimu tukiwa na viongozi wawili wanawake, makamu wa rais na rais tumekutana hapa katika ikulu Dar es Salaam”

Katika ziara hiyo, pia Kamala Harris alitoa heshima kwa waathirika wa shambulizi baya la bomu la mwaka 1998 katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG