Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:34

Marekani inashirikiana na Kenya katika sekta ya kilimo


shamba la mahindi
shamba la mahindi

Kwa miaka mingi, Kenya ilikuwa ikitegemea uagizaji wa mbolea na mahitaji ya nafaka kutoka Russia na Ukraine. Lakini vita vinavyoendelea nchini Ukraine, vimeilazimisha Kenya kuchukua hatua za kujitosheleza yenyewe.

Uvamizi wa Russia nchini Ukriane. Umesababisha sekta ya kilimo kuathirika,na unaendelea kusababisha uhaba wa bidhaa muhimu katika nchi za Afrika kama Kenya, ambazo zinategemea uagizaji wa nafaka, mbolea na vifaa vya kilimo kutoka Ukraine.

Ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali ya Marekani inashirikiana na kampuni za kilimo nchini Kenya ili kuiimarisha sekta hiyo.

Shirila la kimataifa la maendeleo la Marekani USAID, limesema kwamba ni muhimu sana kuwekeza katika kilimo ili kupunguza athari za uhaba wa chakula kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wa Kenya.

David Gosney ni mkurugenzi wa USAID nchini Kenya.

"Kuna kazi kubwa ya kufanya. Kuna umuhimu wa kuzingatia teknolojia mpya ili kuhakikisha kwamba kuna mbegu na mbinu nyingine za uzalishaji. Tumezungumzia pia kuhusu kilimo cha kutumia umeme wa jua kwa ajili ya kunyunguzia mimea mashambani, pamoja na mbinu nyingine zinazoweza kufanikisha kilimo."

Wamiliki wa kampunzi zinazotengeneza mbolea nchini kenya kama David Auerback ameiambia sauti ya Amerika kwamba kampuni yake ya Sanergy itaongeza uzalishaji wa mbolea asili.

Alipewa dola milioni 1.2 kw aajili ya kuzalisha mbolea kwa wakulima wa nchini Kenya.

"Kuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea hapa nchini ni kitu chenye thamani sana. Mbolea yetu ya asili inaongeza uzalishaji wa chakula kwa asilimia 30. Tunafanya kazi kwa kushirikiana na karibu wakulima 10,000 na maduka 1,000 ya kuuza pembejeo katika kila kaunti nchini Kenya na ushirikiano ambao tumuepata kutoka USAID, utatuwezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji na kufikia wakulima wengi kwa haraka."

Marekani ilitangaza kutoa kiasi cha dola milioni 5.1 kwa ajili ya kampuni za kilimo nchini Kenya katika mkutano wa biashara uliofanyika jijini Nairobi, Jumatatu.

Waziri wa biashara na uwekezaji nchini Kenya Moses Kuria, aliuambia mkutano huo kwamba sera za Kenya na Marekani zimekuwa muhimu sana katika ushirikiano huo.

"Ni mpango wa ushirikiano kwa sababu tunashauriana kwa kuzingatia sera zetu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, utandawazi na biashara kupitia mfumo wa digitali."

Makamu rais wa Marekani Kamala Harris amekuwa katika ziara ya wiki nzima Afrika. Amesema kwamba Marekani itaongeza uwekezaji barani Afrika na kusaidia katika ukuaji wa uchumi.

Harris ni afisa wa tano wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani kulitembelea bara la Afrika mwaka huu.

XS
SM
MD
LG